TIZAMA GROUP, tunalenga kumwezesha kila mwanachama kuwa na afya njema, uchumi imara na maisha bora.
TIZAMA GROUP ni kikundi kilichoanzishwa na marafiki waliounganisha mawazo, nguvu na mipango yao kwa lengo la kujenga mfumo wa pamoja wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Kikundi kinalenga kujenga mshikamano miongoni mwa wanachama, kuanzisha miradi, kuwekeza pamoja, kukopeshana na kusaidiana katika changamoto mbalimbali za maisha.
Njia tunazotumia kujenga maendeleo ya pamoja.
Kuimarisha mfumo wa kusaidiana wakati wa changamoto za kiafya
Kuongeza uwezo wa kifedha wa wanachama kupitia mikopo na biashara.
Kuweka rasilimali pamoja kwa ajili ya uwekezaji wa muda mrefu.
TIZAMA GROUP ina utaratibu wa kusaidiana katika matukio mbalimbali kwa mujibu wa Katiba ya Kikundi.
Mtaji mdogo leo unaweza kuwa mwanzo wa hatua kubwa kesho.
"Taarifa hizi ni kwa mujibu wa masharti ya mkopo yaliyopo kwenye Katiba ya TIZAMA GROUP na yanaweza kutegemea masharti na maamuzi ya kikundi."
Tembelea tovuti Login na Utume maombi ya mkopo.
Kamati itapitia vigezo na udhamini na kuthibitisha ombilako.
Ndani ya masaa 72, Mkopo unaidhinishwa na uongozi kisha tatumiwa kwenye Akaunti Ulio elekeza.
Lengo la TIZAMA GROUP ni kujenga uwezo wa kifedha kupitia miradi na uwekezaji wa pamoja.
Kuanzisha biashara zenye uwezo wa kuzalisha mapato ya kila mwezi.
Kuwekeza katika ardhi kama sehemu ya kujenga mali za kudumu za kikundi.
Kutafuta na kutathmini fursa mpya za kibiashara na masoko.
Mfumo wa mzunguko wa fursa za mikopo kwa wanachama kukuza biashara zao.
Kuanzisha mradi wa uzalishaji utakaowezeshwa na mfuko wa kikundi.
Kununua viwanja kwa ajili ya wanachama na umiliki wa kikundi.
Katika kipindi cha miaka mitano, TIZAMA GROUP inalenga kujenga kikundi chenye uwezo mkubwa wa kifedha, miradi endelevu na uwekezaji wa pamoja.
TIZAMA GROUP inaongozwa na viongozi waliochaguliwa kwa misingi ya demokrasia na wanaowajibika kwa wanachama.
Katiba ndiyo msingi wa uendeshaji wa TIZAMA GROUP na inaeleza wanachama, viongozi, malengo, sheria na uwekezaji.
[Namba ya Mawasiliano]
[Email ya Kikundi]
[Mahali / Makao ya Kikundi]
Umoja wetu leo ndio msingi wa mafanikio yetu ya kesho. Jiunge nasi leo katika safari ya maendeleo.